Kulingana na mamlaka za afya, watu 29 wameuawa kusini mwa ukanda huo wakati 16 wameuawa kwenye mji wa Deir al-Balah. Watu wengine 14 wameripotiwa kuwa wameuawa katika maeneo wanajeshi wa Israel waliko karibu na eneo la kugawa misaada.

Boti ya mwisho ya kupeleka misaada Gaza yazuiwa na Israel

Hayo yanajiri wakati waratibu wa boti za kupeleka misaada Gaza wakisema Israel imeizuia boti ya mwisho leo Ijumaa. Boti hiyo imezuiwa ikiwa umbali wa karibu kilomita 78 kutoka Gaza. Taarifa hiyo imetolewa kupitia chaneli ya Telegram ya waratibu wa misaada na kuongeza kuwa jeshi la Israel imezizuia boti zote 42 zilizokuwa zikipeleka misaada Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *