Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa “X” wameuita msafara wa kimataifa wa meli nyingi wa Sumud kuwa meli ya ukarimu na utu wa binadamu.

Msafara wa kimataifa wa Sumud ulitangaza Jumatatu kwamba zaidi ya meli 40 zilizobeba misaada ya kibinadamu ziko njiani kuelekea katika Ukanda wa Gaza, hatua ambayo haijawahi kushuhudiwa inayolenga kuvunja mzingiro wa eneo hilo na kupeleka misaada kwa Wapalestina milioni 2.4.

Wakati huo huo, vyanzo vya habari vimeripoti kuwa, msafara huo umeshambuliwa  na ndege zisizo na rubani katika Bahari ya Mediterania.

Kulingana na Pars Today, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa “X” wamechapisha machapisho mbalimbali yanayoelezea meli za msafara wa Sumud kama ishara ya utu wa binadamu.

Kuhusiana na hilo mwanaharakati wa kisiasa Ali Bahadori Jahromi ameandika kuwa meli za kimataifa zimeonyesha ustahimilivu na zimemfanya kila mtu afanye jambo katika hali yoyote ile. Kwa mujibu wa maneno ya Imam Khomeini, muasisi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ikiwa kila Muislamu atamwaga ndoo moja ya maji, Israel itasombwa na maji. Kadiri tuwezavyo, tunapaswa kuwa wasaidizi wa mnyonge na kuwa adui wa dhalimu.

“Yousef Al-Khawaja,” mtumiaji mwingine wa X, aliita meli za Sumud kuwa ni meli imara na akasema: “Hatupaswi kuwaruhusu Wazayuni kuwaweka watoto wetu kwenye ukatili kupitia mashambulizi ya ndege zisizo na rubani dhidi ya msafara wa Sumud. “Kimya basi.”

“Sara Rezaei” pia amesema: “Waliomo katika meli ya uthabiti na heshima ya wanadamu ni wenzetu ambao wako kwenye sayari inayoitwa Dunia.”

Mohebi, mwanaharakati mwingine wa X, alichapisha video ya watu wa Tunisia wakiukaribisha msafara wa Sumud na kuandika: “Kwa miaka mingi, watu wa dunia waliona mashujaa wa kubuni wa Hollywood, lakini wakati huu wanakumbatia mashujaa wa kweli; mashujaa waliozaliwa kwa imani, mapenzi, na muqawama.”

“Asmaa Hosseini anaamini: “Serikali zinapokaa kimya, watu huingia baharini; Msafara wa Sumud ni sauti ya kimataifa kwa ajili ya Gaza.”

“Kila mtu aliye huru na mwenye heshima anapaswa kuunga mkono msafara wa kimataifa wa misaada wa Sumud kwa nguvu zake zote, na kueneza habari zake katika nchi zote na kupitia majukwaa yote yaliyopo. Pengine Mungu ataufanya msafara huu wa meli za misaada kuwa sababu ya ulimwengu kuinuka kuokoa Gaza na watu wake,” alisema Malik al-Yahmadi.

Mtumiaji aitwaye “Bredrise” ametoa wito kwa watu duniani kote kujitokeza barabarani na kuandamana mbele ya balozi za Israel na Marekani katika nchi zao ili kuongeza shinikizo la kukomesha vita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *