Chama cha ADC kimeahidi kuanzisha mfuko maalum wa kuwafidia wakulima wanaopata hasara wakati wa uzalishaji wa mazao mbalimbali visiwani Zanzibar ili kuendelea na shughuli hizo na kujikimu kimaisha wakati wa majanga hayo iwapo itapata ridhaa ya wananchi ya kushika dola kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29.
Ahadi hiyo imetolewa na mgombea Urais wa chama hicho, Hamad Rashid Mohamed katika kampeni zilizofanyika leo kwenye eneo la Kigunda mkoa wa Kaskazini Unguja kama anavyoeleza Ali Issa.
#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi