Chama Cha Mapinduzi kupitia mgombea wake wa urais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema Ilani ya chama chake kwa mwaka 2025/30 imeweka mkazo katika kuimarisha mawasiliano vijijini na kukuza matumizi ya TEHAMA kama nyenzo muhimu ya maendeleo.
Akizungumza leo mjini Babati katika mkutano wa kampeni, Dkt. Samia ameeleza kuwa serikali ya awamu ya sita tayari imefanikisha ongezeko la upatikanaji wa huduma za simu kutoka asilimia 83 hadi 93, kupitia ujenzi wa minara 5 Hanang, 17 Simanjiro na 21 Kiteto.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates