#HABARI: Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kupitia Chama Cha Mapinduzi, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akiwa wilayani Liwale, mkoani Lindi, kwenye kampeni za kunadi sera za chama hicho, amewaambia wananchi wa wilaya hiyo kuwa Mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CCM Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kipindi cha uongozi wake ameonyesha nia ya kuendeleza sekta ya kilimo kwa kuboresha zoezi la ruzuku ya pembejeo, ili kuwapunguzia makali wakulima na waweze kunufaika na kilimo chenye tija.

Aidha Balozi Dkt. Nchimbi, amesema ndani ya miaka mitano inayokuja endapo watapata ridhaa ya kuongoza nchi, Serikali ya CCM, itajenga skimu mpya za umwagiliaji tano pamoja na kukarabati skimu zote zilizopo eneo hilo na kufanya kilimo chao kisitegemee mvua.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *