#HABARI: Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), mkoani Pwani, wapo katika hatua za kusitisha mikataba ya makandarasi wawili wa kampuni ya Haricom International Ltd na Trinity Manufacturing Services kwa kushindwa kutekeleza ujenzi wa miradi ya miundombinu ya barabara kwa wakati.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhandisi Rogatus Mativila, ameyasema hayo alipokagua utekelezaji wa barabara Rufiji mkoani Pwani.
Mativila amezitaja kampuni hizo kuwa ni Trinity Manufacturing Services, ambayo toka Agosti mwaka jana hajatengeneza barabara hiyo huku Haricom akitakiwa kuanza ujenzi huo Aprili 10 mwaka jana lakini hadi sasa hakuna utekelezaji wowote wa kazi hiyo.
Amesema tayari serikali imewalipa fedha nyingi kuanza ujenzi huo ambapo kampuni ya Trinity ililipwa shilingi milioni 460 malipo ya awali tangu Agosti mwaka jana na ulitakiwa uwe umekamilika mwaka huu mwezi Novemba huku kampuni ya Haricom International Ltd, aliyepewa kazi ya utengenezaji wa barabara ya Polisi – Kirungi yenye urefu wa Kilomita moja, ambao walitanguliziwa kiasi cha shilingi milioni 160 lakini hadi sasa hawajatekeleza huku vifaa vya ujenzi vikiwa vimetelekezwa katika eneo la mradi.
Ameongeza kuwa kampuni hiyo hadi kukamilika kwa mradi huo gharama zake ni kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni sabini fedha ambazo zinatokana pia na kodi za wananchi.
Amesema kutokana na kushindwa kutekeleza miradi hiyo mhandisi Mativila ameagiza makandarasi hao wasipewe kazi zozote kupitia Tamisemi.
Kwa upande wake Meneja Tarura mkoani Pwani Mhandisi Ibrahim Kibasa amesema licha ya jitihada za kuwatafuta makandarasi hao kwa njia tofauti lakini amekwama kutokana na kukosa ushirikiano kwa upande wao.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KISHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.