#HABARI:Aliyekua Mbunge wa Viti maalum Cecilia Paresso ameshangazwa na baadhi ya wanasiasa waliosusia uchaguzi, ambao ni huru na wa haki, licha ya vyama 18 kushiriki uchaguzi, ambapo amewataka wananchi wilayani Karatu mkoani Arusha kujitokeza Oktoba 29, na kumchagua mgombea urais wa CCM Dkt.Samia Suluhu Hassan, ili aweze kuwaletea watanzania maendeleo makubwa.