
Iran imesema wanaume hao waliwaua maafisa wa polisi na vikosi vya usalama, pamoja na kupanga mashambulizi ya mabomu yaliolenga maeneo karibu na mji wa Khorramshahr, katika mkoa wa Khuzestan nchini Iran.
Televisheni ya taifa ya Iran ilipeperusha hewani picha za mmoja wa watu hao akizungumzia mashambulizi hayo, akisema ni mara ya kwanza kwa maelezo hayo kutolewa hadharani.
Mauaji ya wafungwa yanakuja baada ya vita vya Israel na Iran
Mauaji hayo yanafuatia vita vya siku 12 vya Iran na Israel mwezi Juni, vilivyomalizika huku Tehran ikiapa kuwa itawaandama maadui zake ndani na nje ya nchi.
Hata hivyo, wanaharakati wanaonya kuwa Iran mara nyingi hutegemea kukiri kwa kulazimishwa na kesi za faragha katika hukumu yake ya kifo hasa zile zinazoihusisha Israel.