Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeteketeza jumla ya kilogramu 4,402.02 za dawa za kulevya katika kiwanda cha saruji cha Twiga, kilichopo Wazo, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza kabla ya zoezi hilo, Kamishna Jenerali wa DCEA, Aretus Lyimo amesema dawa zilizoteketezwa ni pamoja na kilogramu 2,168.18 za methamphetamine, 1,064.29 za heroin, gramu 326.95 za cocaine, kilogramu 515.48 za bangi, na kilogramu 653.74 za mirungi.

Amebainisha kuwa dawa hizo zilikuwa vielelezo vya mashauri mbalimbali yaliyokuwa yakisikilizwa mahakamani, ambapo mengine tayari yamehitimishwa kwa hukumu. Kamishna Lyimo ameongeza kuwa kwa mashauri ambayo bado hayajakamilika, mahakama imetoa ruhusa ya kuteketeza dawa hizo kutokana na hatari ya kuharibika au kubadilika umbo.

#AzamTVupdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *