Mgombea urais wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameahidi kutatua changamoto ya magugu maji kwenye Ziwa Babati na maziwa mengine nchini yaliyoathiriwa na mimea hiyo, ambayo imeathiri uvuvi na shughuli za kijamii.
Akihutubia leo mjini Babati katika siku ya pili ya kampeni zake mkoani Manyara, Dkt. Samia amesema serikali ya awamu ya sita tayari imetoa fedha za kununua mtambo maalum wa kuondoa mimea hiyo.
Aidha, ameahidi pia kununua boti nne kwa mkoa huo, tatu za uvuvi na moja ya usalama, ili kuboresha mazingira ya uvuvi kwa wananchi.
✍ @claud_jm
#AzamTVUpdates