Mkutano wa 12 wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit) uliowakutanisha wadau mbalimbali wa Sekta ya Afya umehitimishwa Septemba 2, 2025 Jijini Dar es salaam huku ikisisitizwa juu ya umuhimu wa kuzingatia matumizi sahihi ya takwimu na matumizi ya teknolojia katika kufanikisha upatikanaji wa huduma bora za afya nchini.

Akizungumza pembezoni mwa mkutano huo uliowakutanisha washiriki zaidi ya 1,700 kutoka nchi mbalimbali duniani Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Tanzania Health Summit, Dkt. Chakou Halfan Tindwa amesema pamoja na kujadili mambo mbalimbali wameona kuna haja ya kutilia mkazo juu ya matumizi sahihi ya Teknolojia na Takwimu ili kufanikisha azma ya serikali ya kutoa huduma bora za afya kwa kila mwananchi.

Imeandaliwa na Tumie Omary
Mhariri | @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *