
Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa X wamesisitiza haja ya kuwa macho dhidi ya mpango wa Rais wa Marekani wa kusitisha vita huko Gaza.
Duru za habari zilisema kuwa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina “Hamas” imewasilisha jibu lake rasmi kwa mpango wa Rais wa Marekani wa kusimamisha vita huko Gaza kwa wapatanishi. Katika sehemu ya hotuba yake, “Musa Abu Marzouk” mmoja wa viongozi wa Hamas alisema kwamba kipaumbele chetu ni kusimamisha vita na uhalifu, na kwa hiyo, tumeonyesha ushirikiano chanya kwa mpango huu.
Abu Marzouk aliuchukulia mustakabali wa taifa la Palestina kuwa ni suala la kizalendo ambalo Hamas peke yake haiwezi kuamua juu yake. Kwa mujibu wa Pars Today, watumiaji wa mtandao wa kijamii wa “X” wamesisitiza kuwa, kwa kuzingatia hatua ya Marekani ya kukiuka ahadi zake na ukiukaji wa mara kwa mara wa usitishaji vita unaofanywa na Wazayuni, mtu anapaswa kuwa macho sana dhidi ya mpango huo wa Rais Donald Trump wa Marekani.
Kuhusiana na hili, mtumiaji mtandao wa X anayeitwa “Farid Hamdard” aliandika: “Si Trump ni mwaminifu wala Hamas si harakati ya kuchukulia mambo kiwepesi wepesi. Hakuna amani wala usitishaji wa kudumu wa mapigano. Hivi ni vita ambavyo upande mmoja unapaswa kuangamizwa, na upande huo bila shaka ni Wazayuni. Kuangamizwa kwa Israel kuna uwezekano mkubwa, Inshallah.”
Katika sehemu ya chapisho la Amir Ali Abu al-Fath, mtaalamu wa masuala ya kisiasa imeelezwa kuwa, iwapo nchi zote za Kiislamu zitafikia amani na Israel, amani haitapatikana Palestina hadi pale Wapalestina watakapoonja uadilifu. Trump hawezi kufanya lolote peke yake madhali Israel haijataka haki kwa Wapalestina.
“CESÎM ZEYDAN,” mtumiaji mwingine wa X, alisema: “Hamas imeiweka pembeni na kuitenga Israel kidiplomasia baada ya kufedheheshwa kijeshi. Kwa maoni yangu, mauaji ya halaiki yanaweza yasimalizike, na hata yakiisha, Israel huenda ikakiuka usitishaji vita. Kwa vyovyote vile, Israel imepata pigo la kufedhehesha.”
“Mohammed Abu Zar” pia alisisitiza: “Sisi, watu wa Palestina, tunasimama na wapiganaji wa muqawama wa Hamas katika kila uamuzi wanaoufanya. Uhai kwa muqawama, uhai kwa Hamas.”
Hiyuman pia maesema: “Waisraeli wanashambulia kwa mabomu na kuwapiga risasi raia hata zaidi baada ya Hamas kukubaliana na makubaliano ya Trump. Waisraeli ni magaidi kwa sababu daima wanasema uongo na kisha huharibu kila mpango wa amani katika ulimwengu huu.”
Na hatimaye Saad Al-Hamzamani amebainisha pia kwamba watu madhulumu wa Ghaza wasifikirie kuwa mpango wa Trump ndio utakaomaliza mauaji na uharibifu wa eneo hili. Mpango huu ni ujanja tu wa kuwaachilia wafungwa wa Kizayuni katika hatua ya kwanza.