Serikali imeombwa kutoa muongozo mpya kwa wamiliki wa maduka ya vipodozi ikiwemo kutungwa kwa sheria itakayowabana wauzaji ili kuhakikisha wanakuwa na sifa zinazoendana na shughuli za uuzaji wa dawa muhimu ili kulinda afya za wananchi.

Wito huo umetolewa jijini Mwanza kufuatia madai ya kuwepo kwa wauzaji wa maduka ya vipodozi wasiokuwa na weledi na wanaotoa ushauri bila kufahamu hali kiafya za wateja na viambata vilivyopo kwenye dawa.

Innocent Aloyce ana taarifa zaidi.

#AzamTVUpdates
Mhariri | @moseskwindi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *