Tafiti zimebaini kuwa ukosefu wa miti ya kutosha katika mashamba unasababisha upotevu mkubwa wa maji, jambo linaloweza kuchochea ongezeko la magonjwa yanayohusiana na joto, ikiwemo magonjwa ya figo.
Akizungumza katika mkutano wa 12 wa Afya Tanzania (Tanzania Health Summit), Mratibu wa Mradi wa KISHADE, Gumi Mrisho, amesema matokeo ya utafiti huo ulioongozwa na shirika la LEAD Foundation kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na Hospitali ya Taifa Muhimbili yanaonesha umuhimu wa kulinda mazingira kwa kupanda miti ili kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi na kulinda afya za wakulima.
#AzamTVUpdates
✍Rebeka Mbembela
Mhariri | John Mbalamwezi