Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka ili kuzuia mauaji makubwa ya kikabila yanayoendelea kutekelezwa kwenye mji wa El-Fasher, magharibi mwa Sudan.

Wito huu umetolewa baada ya Ofisi ya Tume ya Haki za binadamu kueleza katika ripoti yake kueleza kuwa mashambulio yakiongozwa na wanamgambo wa RSF yameongezeka katika eneo hilo, na kuzua wasiwasi wa mashambulio makubwa Kaskazini mwa Darfur, katika siku za hivi karibuni. Taarifa ya Volker Turk Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu, imesema mauaji makubwa yanayoendelea pamoja na mateso, yanapaswa kukoma.

Kati ya tarehe 19 hadi 29 mwezi Septemba, Tume hiyo ya Haki za binadamu, imesema, watu 91 waliuwa baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa RSF, kwa kile kinachoonekana ni kuwaondoa wakaazi wa El Fasher.

 Umoja wa Mataifa, unataka raia wa kawaida kulindwa kwenye mji huo, hasa wale wasiokuwa na uwezo kuondoka El-Fasher, na kuwataka wanamgambo wa RSF na jeshi la Sudan, kukubali misaada ya kibinadamu kuwafikia wenye uhitaji. Wakati huo huo, watu wapatao 91 wameuawa katika mji wa El-Fasher uliokuwa umezingirwa na wanamgambo wa RSF, kufuatia mashambulizi makali yaliyofanywa na wanamgambo hao na yaliyodumu kwa siku kumi mwezi uliopita.

Kwa mujibu wa Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu, Volker Türk, kitongoji cha Daraga Oula kilichopo magharibi mwa El-Fasher kimekuwa kikilengwa mara kwa mara na mashambulizi ya RSF, yakihusisha matumizi ya mabomu, droni, na uvamizi wa ardhini kati ya Septemba 19 hadi 29.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *