
Katika chapisho kwenye mtandao wake wa Truth Social, Trump amesema anaamini Hamas iko tayari kwa amani ya kudumu na akaitaka Israel ikomeshe mara moja mashambulizi ya mabomu Gaza.
Kwa upande wake, waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema kwa kuzingatia majibu ya Hamas, Israel inajiandaa kwa ajili ya utekelezaji wa haraka wa hatua ya kwanza ya mpango wa Trump wa kuwaachilia mateka wote.
Wakati huo huo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Qatar Majed al-Ansari, amepongeza tangazo hilo la Hamas na kuelezea kuunga mkono wito wa Trump wa kusitishwa kwa mapigano mara moja.
Naye kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, amesema mpango wa Trump unawakilisha fursa bora zaidi ya amani katika mzozo huo.