
WADA imesema kutokana na juhudi hizo za Kenya, tishio la adhabu husika halikuanza kutekelezwa kufikia muda huo wa mwisho hapo jana.
Suala hilo kuhusu Kenya, limerejeshwa kwa idara ya uzingatiaji wa kanuni ya WADA, ambayo itaangalia upya utendakazi wa Shirika la Kenya la Kupambana na Matumizi ya Dawa za Kusisimua Misuli (ADAK), na kutoa masasisho.
ADAK yashtumiwa kwa kutokidhi viwango
Mwezi uliopita, WADA yenye makao yake makuu mjini Montreal nchini Canada, ilisema kuwa tawi lake la Kenya halikidhi viwango vyake na kulipa hadi jana Ijumaa, Oktoba 3, kushughulikia masuala hayo.
Siku ya Alhamisi, Rais wa Kenya William Ruto, alisema nchi hiyo itafanya kila kinachohitajika kuleta mabadiliko katika utendakazi wa (ADAK), kuepusha adhabu ambazo zinaweza kuwazuia wanariadha wake kushiriki mashindano chini ya bendera ya Kenya.