
Afisa mkuu wa polisi nchini Ujerumani Dieter Romann.Romann ameliambia gazeti la Welt am Sonntag, lililoonekana mapema na vyombo vya habari hii leo kwamba mwaka jana pekee, walisajili safari za kuwarejesha makwao wahamiaji 53,800 na kati ya hao, takriban safari za wahamiaji 33,600 zilifutiliwa mbali kabla ya wahamiaji hao kufikishwa katika vituo vya vizuizi.
Ukosefu wa vizuizi vya wahamiaji ni tatizo kubwa
Pia amekosoa ukosefu wa vituo vya vizuizi vya wahamiaji nchini Ujerumani.
Roman amesema, wakati watu 226,000 wanatakiwa kuondoka nchini humo lakini kuna chini ya vituo 800 pekee vya vizuizi, polisi wa serikali na shirikisho wataendelea kushindwa kuwaweka vizuizini wahamiaji hao wanapopatikana, hata kama vigezo vya kisheria vimefikiwa.