
Polisi imesema wanaume watatu na wanawake watatu, wenye umri wa kati ya miaka 18 na 60, walikamatwa katika eneo la Manchester kwa tuhuma za kupanga na kutekeleza vitendo vya kigaidi.
Shambulizi hilo limeitia hofu jamii ya Wayahudi wa Uingereza na kuzidisha mjadala kuhusu ukosoaji wa Israel na chuki dhidi ya Wayahudi.
Maandamano dhidi ya Israel yachochea chuki dhidi ya Wayahudi
Baadhi ya wanasiasa na viongozi wa kidini wanadai kuwa maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina ambayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara tangu kuanza kwa vita vya Gaza, yamechangia katika kueneza chuki dhidi ya Wayahudi.
Maandamano hayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa ya amani lakini wengine wanasema nyimbo kama vile “Kutoka
mto hadi baharini, Palestina itakuwa huru” zinachochea chuki dhidi ya Wayahudi.