
Watu waliokimbia makazi yao kutokana na vita wanalengwa na makundi yenye silaha. Haya ndiyoyanajiri kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambapo Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, unalaani kuongezeka kwa ghasia katika mkoa huoa Ituri, ambapo watu 14 waliokimbia makazi yao waliuawa Oktoba 2 na kundi la wapiganaji la Cooperative for the Development of Congo (CODECO), kwa mujibu wa MONUSCO. Eneo lililolengwa ni makazi ya maelfu ya raia wanaokimbia ghasia.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu wa Kinshasa, Pascal Mulegwa
“Shutma,” “uchunguzi,” “kuwafikisha wahusika mbele ya sheria” -hayani baadhi ya maeneo yalio kwenye taarifa ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO), lakini yanaonyesha wasiwasi unaoongezeka wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo.
Watu hao 14 waliuawa katika eneo la Roho, katika mji wa Maze, walipokuwa wakienda kufanya kazi mashambani. Kulingana na mashirika ya kiraia ya eneo hilo, washambuliaji waliwavizia, wakafyatua risasi, na kuwajruhi baadhi yao kwa visu. Hata hivyo, MONUSCO inabainisha kwamba hasara hizi zilitokana na mapigano kati ya makundi yenye silaha ya Cooperative for Development of Congo (CODECO) na Zaire, kila upande ukidai kulinda jamii yake dhidi ya mwenzake.
Ujumbe huo unaripoti vifo vya angalau saba kati ya pande hasimu. Usiku huo huo, huko Gina, yapata kilomita thelathini kutoka Bunia, milio ya risasi iliyohusishwa watu wasiojulikana wenye silaha iliwalazimu karibu raia 2,500 kutafuta hifadhi katika kituo cha walinda amani.
Ujumbe wa Umoja wa Mataifa unaelezea vitendo hivi vya unyanyasaji kama “visivyoweza kuelezeka” na vinaweza kuwa ukiukaji mkubwa wa sheria za kimataifa za kibinadamu na sheria za haki za binadamu. Vivian van de Perre, naibu mkuu wa MONUSCO, anasisitiza kuwa uwepo wa Umoja wa Mataifa umeimarishwa katika maeneo nyeti, lakini analaani mapigano karibu na maeneo ya watu waliotoroka makazi yao, ambayo yanawaweka hatari watu hawa.