
Khalil al-Hayya kiongozi wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amejitokeza kwa mara ya kwanza tangu utawala wa Israel ulipowashambulia huko Doha maafisa wa harakati hiyo ya Muqawama ya Palestina.
Kiongozi huyo wa muqawama anayeongoza timu ya mazungumzo ya Hamas jana aliwahutubia wananchi wa Palestina ambapo alitoa maoni yake kuhusu mauaji kuhusu kuuliwa shahidi wenzao sita katika hujuma ya kigaidi ya Israel huko Doha akiwemo mwanawe wa kiume kwa jina la Hammam, meneja wa ofisi yake, Jihad Labad, na wawakilishi kadhaa wa ofisi yake, mnamo Septemba 9 mwaka huu.
“Leo tunaishi katika kivuli cha maumivu na wakati huo huo katika kivuli cha fakhari na heshima,” amebainisha Khali al Hayya,”.
Kiongozi huyo wa ngazi ya juu wa Hamas ameeleza kusikitishwa kuuawa shahidi kwa wanamapambano wenzao lakini akasema bado anajisikia fakhari mkabala wa wahanga hao ikiwa ni pamoja na mtoto wake ambao walisabilia maisha yao wakipambana kulikomboa taifa la Palestina kutoka mikononi mwa uvamizi na kukaliwa kwa mabavu na Israel inayoungwa mkono kwa hali na mali na Marekani.
“Siwezi kutofautisha kati ya wahanga hawa na mtoto yoyote wa Kipalestina huko Gaza ambaye ameuawa shahidi na utawala vamizi,” amesema kiongozi wa ngazi ya juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas).
Hayya pia Hayya amepongeza mapambano ya Wapalestina ya zaidi ya karne moja dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni na njama za Wamagharibi zenye lengo la kuuimarisha utawala huo ili kufanikisha malengo yake hatari ya kujitanua pakubwa huko Palestina.