Mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Jimbo la Kigoma Kusini, Nuru Kashakari (Kandahari), ameahidi kujenga kituo cha afya ndani ya miezi sita baada ya kuapishwa, akitumia fedha zake binafsi, ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi ambao kwa sasa wanalazimika kusafiri zaidi ya saa nne kufuata huduma hizo.
Akizungumza katika kijiji cha Rukoma, Kata ya Igalula, ‘Kandahari’ aliwahimiza wananchi kumchagua yeye pamoja na Dkt. Samia Suluhu Hassan kama Rais wa Tanzania, akisisitiza kuwa miradi mikubwa iliyotekelezwa katika jimbo hilo katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais huyo ni ushahidi tosha wa maendeleo yanayoendelea kuletwa kwa wananchi wa Kigoma Kusini.
✍ Jacob Ruvilo
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates