
Chama cha Conservative cha Uingereza kinakutana leo Jumapili, Oktoba 5, mjini Manchester kwa mkutano wake wa kila mwaka. Baada ya kuongoza serikali kwa miaka 14, Tories ilipata moja ya hasara mbaya zaidi katika historia yao mnamo mwaka 2024. Kwa kipindi cha mwaka mmoja, chama hiki kilipoteza wanachama 10,000. Mkutano huu unapaswa kuruhusu chama kujijijenga tena kama chama cha serikali, lakini kufikia katika hatua hiyo bado kina kazi kubwa ya kufanya.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mkutano huu unaadhimisha kumbukumbu ya mwaka wa kwanza wa Kemi Badenoch kama kiongozi wa Chama cha Conservative. Lakini katika muda wa mwaka mmoja, kiongozi wa upinzani ameshindwa kuimarisha Tories, anaripoti mwandishi wetu wa London, Emeline Vin.
Tatizo la kwanza: kuibuka kwa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Reform. Katika mkutano wa chama mapema mwezi Septemba, kiongozi wake, Nigel Farage, akichochewa na mafanikio yake katika uchaguzi, alitangaza nia yake ya kuhamia 10 Downing Street. Kila wiki, Wahafidhina mashuhuri hutangaza kujitoa kwao kwa chama kinachotetea utaifa, kinachopinga uhamiaji, ambacho Chama tawala cha Labour sasa kinakichukulia kuwa mpinzani wake mkuu.
Matokeo: Kemi Badenoch anatoa mlolongo wa ahadi za kisiasa za mrengo mkali wa kulia : kuachana na malengo ya mazingira, kuimarisha sheria za uhamiaji, kuvunja uhusiano na Mahakama ya Ulaya ya Haki za Kibinadamu… Wahafidhina wenye msimamo wa wastani zaidi, katikati-kulia, hawako tena katika chama chenye mti wa buluu. Wanachama wakuu wana wasiwasi kuhusu kupungua kwa idadi ya wapiga kura iliyotabiriwa.
Mbali na wafuasi, siku hizi nne za kongamano huko Manchester zinafaa pia kurejesha uaminifu kwa chama ambacho kimekumbwa na kashfa nyingi katika miaka ya hivi karibuni, kuanzia na zile zilizochafua muhula wa Waziri Mkuu wa zamani Boris Johnson. Kulingana na YouGov, karibu Waingereza sita kati ya kumi wanaamini kuwa Tories kitakuwa chama kidogo katika mhali ya kisiasa inayojiri kwa sasa.