Mgombea wa Urais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amewahakikishia wananchi kuwa katika kipindi cha awamu ya pili ya serikali yake, itapunguza gharama za chakula kupitia mpango wa kununua mpunga na mahindi ya kutosha kutoka Tanzania Bara.

Dkt. Mwinyi amewaomba wananchi wampe ridhaa ya kuendelea kuongoza, akibainisha kuwa serikali yake imejipanga kusimamia bei za vyakula zisipande tena. Aidha, ameeleza mipango ya kuondoa changamoto za mfumuko wa bei kwa kujenga bandari ya Shumba, itakayowezesha meli kubwa kutoka nje ya nchi kushusha vyakula moja kwa moja kisiwani Pemba.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *