Nahodha na mshambuliaji wa Argentina, Lionel Messi huenda asiwe sehemu ya kikosi cha Argentina kitakachocheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Venezuela na Puerto Rico.

Messi mwenye umri wa miaka 38, alicheza mechi moja tu kati ya mbili za mwezi Septemba 2025, kabla ya kupewa ruhusa kurejea kwenye Klabu yake ya Inter Miami.

Kocha mkuu wa Argentina, Lionel Scaloni, amesema hana nia ya kuhatarisha afya ya mchezaji yeyote kwenye mechi hizo mbili, ikiwa ni pamoja na Messi.

Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Scaloni amesema: “Tutazungumza naye (Messi) na wachezaji wote. Wazo letu si kuhatarisha afya ya mchezaji yeyote.

MES 01

“Hizi ni mechi za kirafiki, na bila shaka timu ya taifa ni muhimu, lakini kama mchezaji atakuwa na tatizo hata dogo kama ilivyo kwa Marcos Acuña hatutamtumia. Lakini kama atakuwa fiti, basi atacheza.”

Messi amekuwa na kipindi kigumu cha kucheza mechi nyingi mfululizo akichezea Inter Miami, akimaliza msimu wa kawaida wa Ligi ya Marekani (MLS) kwa kiwango cha juu.

MES 02

Amefunga mabao 24 na kutoa pasi za mabao 17, na kusaidia timu yake kufuzu hatua ya mtoano (playoffs) kwa mwaka wa pili mfululizo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *