Lisbon, Ureno. Shirikisho la Soka Barani Ulaya (UEFA) linafanya mpango mpya wa kufanya hatua za kufuzu kwa Mashindano ya Ulaya (Euro) ziwe za kuvutia na za burudani zaidi kwa mashabiki.
Rais wa UEFA, Aleksander Ceferin, amesema hana nia ya kubadilisha mashindano yenyewe, lakini amekiri hivi karibuni kwamba hatua za kufuzu zinaweza kufanyiwa marekebisho na kuboreshwa.
“Pengine hatua za kufuzu zinaweza kuwa tofauti,” Ceferin alisema alipokuwa akizungumza katika Mkutano wa Soka wa Ureno 2025.
“Hakutakuwa na mechi zaidi, bali mfumo wa kuvutia zaidi. Tunaliwazia hili kwa sasa.”
Tathmini ya ndani ya UEFA kuhusu jinsi ya kuwavutia mashabiki wakati wa kampeni za kufuzu inatarajiwa kuzingatia njia mbadala kadhaa.
Inawezekana UEFA ikaangalia mifumo ya kufuzu inayotumika katika mashindano mengine kama UEFA Nations League au UEFA Champions League.
UEFA haikutaka kutoa maelezo ya kina kuhusu mapitio hayo ilipoulizwa na Daily Mail Sport.
Mfumo wa Nations League unahusisha kupanda na kushuka daraja, huku mfumo mpya wa Ligi ya Mabingwa Ulaya ukiwa na timu zinazocheza mechi sita badala ya mfumo wa zamani wa hatua ya makundi ambapo timu zilicheza mechi za nyumbani na ugenini.
Mashabiki wengi wa soka wameanza kukerwa na mapumziko ya ligi ya kupisha mechi za kimataifa – kwani katika miezi mitatu tu ya kwanza ya msimu tayari kuna mapumziko matatu – na sasa inaonekana vyombo vinavyosimamia soka vimeanza kusikiliza malalamiko hayo.
Mapumziko haya ya wiki mbili ya mwezi Oktoba ya kupisha mechi za kimataifa ndiyo ya mwisho katika mfumo huu, kwani kuanzia mwaka 2026 yamepangwa kuondolewa.
FIFA imeamua kuunganisha mapumziko ya wiki mbili-mbili ya Septemba na Oktoba kuwa dirisha moja la mapumziko ya wiki tatu za pamoja, ambapo mataifa yatacheza mechi nne badala ya mbili kama ilivyokuwa awali.
Hatua hii inalenga kuongeza wiki moja zaidi ya mashindano ya ligi za ndani