Madrid, Hispania. Winga wa Real Betis, Antony amefichua kwamba Mbrazili mwenzake, Matheus Cunha alimbebeleza sana kumtaka abaki Old Trafford kabla ya kufanya uamuzi wa kutimkia Hispania.

Antony alinaswa na kocha Erik ten Hag wakati alipotua Manchester United, lakini kiwango chake cha uwanjani kimeshindwa kuendana na pesa iliyolipwa kumsajili, Pauni 85 milioni.

ANTO 02

Wakati Ten Hag alipofunguliwa mlango wa kutokea Oktoba 2024, maisha ya Mbrazili huyo nayo yakaelekea ukingoni. Ujio wa kocha mpya, Ruben Amorim ulimfanya winga huyo kufunguliwa mlango wa kutokea, kwanza akitolewa kwa mkopo kwenda Real Betis.

Ilipofika Januari, Amorim alimtoa kwa mkopo Antony kwenda Betis, mahali ambako aliboresha kiwango chake na kuwa bora uwanjani. Winga huyo alifunga mabao tisa na kuasisti mara tano huko Hispania na kuisaidia timu yake kufika fainali ya Conference League.

Msimu ulipomalizika, Antony alirejea Man United na aliambiwa klabu hiyo inamtaka aondoke. Na staa huyo alifichua Mbrazili mwenzake, Cunha, ambaye alijiunga na Man United akitokea Wolves hakutaka Antony aondoke.

ANTO 01

“Matheus Cunha alitaka mimi tucheze pamoja, lakini mambo yalikuwa magumu,” amesema Antony na kuongeza. “Namkubali sana.”

Wakati dili la Antony kwenda Betis lilipoonekana kama kuwa gumu, staa huyo alikuwa akifanya mazoezi kivyake huko Carrington.

Antony amesema: “Sizungumzi sana na Ruben Amorim. Uamuzi wake wa kunifanya nifanye mazoezi kivyangu, lakini niliheshimu.” Msimu huu, huko Betis, Antony amefunga na kuasisti katika mechi moja ya sare ya 2-2 dhidi ya Nottingham Forest kwenye Europa League.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *