London, England. Kiungo, Martin Zubimendi amefichua kwamba simu moja tu aliyopigiwa na kocha Mikel Arteta ilimfanya ashawishike na kwenda kujiunga na Arsenal kwenye uhamisho wa dirisha lililopita.

Arsenal ilikamilisha uhamisho wa staa huyo wa Kihispaniola kwa ada ya Pauni 51 milioni akitokea Real Sociedad ya huko Hispania.

Simu ya Arteta ndiyo iliyomshawishi Zubimendi kukubali kuachana na Sociedad ikiwa ni miezi 12 baadaye baada ya kukataa ofa ya kwenda kujiunga na Liverpool.

ZUBI 01

Zubimendi, 26, ameanza vyema maisha yake huko London, akiisaidia Arsenal kushuka usukani wa Ligi Kuu England baada ya kucheza mechi saba.

Akizungumza kuhusu ofa ya Liverpool na uamuzi wa kwenda Arsenal, Zubimendi amesema: “Ofa yoyote ilipokuja, swali la kwanza lilikuwa ni ama kubaki Real au kuondoka, wakati ule haukuwa mwafaka.

“Nilibaki na ulikuwa msimu mgumu sana, lakini nilijifunza vingi. Nilitazama mbele inakuwaje na kuacha mambo mengine yapite.”

Katika ishu ya kuichagua Arsenal, Zubimendi amesema: “Niliitazama Arsenal na kupenda kila kitu nilichokiona, katika ishu ya dhamira, vijana na ile ladha ya kuwatazama. Na Mikel Arteta aliponipigia timu. Kama ulishawahi kuzungumza naye, utafahamu, ana ushawishi sana.

“Ni kichaa wa soka, kichaa wa kila kitu akikitaka kukifahamu kwenye mapana yake. Alikuwa wazi kwa kila kitu na mradi aliouweka mezani ulikuwa na ushawishi mkubwa kwangu.”

Zubimendi ameitumikia Arsenal kwenye mechi tisa hadi sasa na amekumbana na kichapo mara moja tu. Staa huyo alionyesha makali yake kwenye mechi dhidi ya Nottingham Forest, ambapo alifunga mara mbili kwenye ushindi wa 3-0. Arsenal itakipiga Jumamosi dhidi ya Fulham.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *