
Dar es Salaam. Mwanadada Nana Shanteel aliyezaa na msanii wa Bongofleva Harmonize, amesema hawezi kumchukia baba wa mtoto wake huyo ambaye wamejaaliwa kupata mtoto mmoja wa kike, Zulekha ‘Zuu’.
Shanteel ameliambia Mwananchi kuwa hawezi kumchukia Harmonize hata siku moja kwa sababu atabaki kuwa ‘baby daddy’ wake ambaye anatimiza vizuri majukumu yake kwa mtoto wao.
“Siwezi kabisa kuongelea uhusiano wangu na Harmonize, kwa sababu hayo ni maisha yangu binafsi, lakini mimi na yeye tupo sawa kwa sababu tunalea mtoto, na kila mmoja kwasasa yupo kwenye uhusiano wake mwingine,” amesema Shanteel.
Aliongeza kusema kuwa habari za kusema Harmonize hatimizi wajibu wake kwa mtoto sio za kweli.
“Achana na habari za watu wanaopenda kuzungumzia maisha ya watu, Harmonize anatimiza vizuri tu majukumu yake kama baba.”
Shanteel amesema pia, kwasasa yeye ameshaolewa na mwanaume mwingine na amejaaliwa kupata mtoto mwingine.
“Mimi nimeshaolewa kitambo na sasa nimebarikiwa kupata mtoto wa kwanza wa kiume kwenye ndoa yangu japo ni mtoto wa pili baada ya Zuu.