Shabiki mmoja wa soka kutoka Ghana, anayejulikana kwa jina la Obour, amezua hisia mitandaoni kufuatia hotuba yake ya kujiamini iliyopeleka ujumbe wa moja kwa moja kwa Rais wa Marekani, Donald Trump, baada ya timu ya taifa ya Ghana, Black Stars, kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2026.

Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa awali na YEN.com.gh, Black Stars ilifuzu kushiriki Kombe la Dunia litakalofanyika Amerika Kaskazini, na kuwa taifa la 21 kujihakikishia nafasi kwenye mashindano hayo makubwa yatakayofanyika kati ya Juni 11 hadi Julai 19, 2026, katika nchini za Marekani, Canada na Mexico.

Ghana ilipata ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Comoros kwenye Uwanja wa michezo wa Accra, juzi Jumapili, Oktoba 12.

SHAB 01

Katika video iliyosambaa hivi karibuni, Obour amezungumzia mipango yake ya kusafiri kwenda Marekani kuishangilia timu yake ya taifa. Amesema kwa msisitizo kuwa utawala wa Donald Trump hautamzuia yeye wala wenzake kusafiri kushuhudia mechi za Ghana.

Kauli hiyo ya Obour imekuja baada ya tangazo rasmi la kuondolewa kwa vikwazo vya viza dhidi ya raia wa Ghana. 

Tangazo hilo lilitolewa na Waziri wa Mambo ya nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa, ambaye alieleza kuwa raia wa Ghana kwa sasa wanaweza kuomba viza ya Marekani ya kuingia mara nyingi kwa kipindi cha miaka mitano.

Hata hivyo, shabiki huyo amesisitiza kuwa wao hawana nia ya kuhamia Marekani kinyume cha sheria za nchi hiyo, bali lengo lao kuu ni kuiunga mkono Black Stars, na kuhakikisha inatwaa ubingwa wa Kombe la Dunia 2026.

SHAB 02

Shabiki huyo amemalizia kwa matumaini makubwa, akisema kuwa timu ya taifa ya Ghana, itapewa fursa nzuri ya kuonyesha uwezo wake katika fainali hizo, zinazosubiriwa kwa hamu kubwa duniani kote.

Ingawa Obour anaamini kuwa mechi za Black Stars zitachezwa Marekani, licha ya tarehe na maeneo halisi ya mechi hizo bado hayajatangazwa rasmi, na yatakuwa wazi baada ya droo rasmi ya makundi kufanyika mwezi Desemba 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *