Papa Leo ameitaka dunia kujitafakari kuhusu mitindo yao ya maisha na vipau mbele vyao.
“Kuwaruhusu mamilio ya binadamu waishi – na kufa – wahanga wa njaa ni kushindwa kwa pamoja na dhambi ya kihistoria,” alisema Papa katika hotuba aliyoitoa katika shirika la Umoja wa Mataifa la kilimo lililo na makao yake huko Roma.
“Janga la njaa linazidi kuikumba sehemu kubwa ya binadamu,” alisema hayo siku moja bada ya Umoja wa Mataifa kutahadharisha kuwa njaa duniani imefikia viwango vya rekodi.
Kiongozi huyo wa dini amezungumzia hali ambapo kiasi kikubwa cha chakula kinatupwa duniani wakati ambapo mamilioni ya watu wanahangaika kupata chochote cha kutia kinywani.
Amezungumzia hasa yanayoendelea “Ukraine, Gaza, haiti, Afghanistan, Mali, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Yemen na sudan Kusini,” miongoni mwa nchi nyengine ambako umaskini umekuwa jambo la kawaida.
Amelaani pia hatua ya ulimwengu kuonekana kusahau suala la njaa kutumika kama silaha ni uhalifu wa kivita.