
Kufuatia harakati za vuguvugu za kisiri za Raila Odinga, sio rahisi kusema ni lini hasa alianza kujiingiza katika siasa, lakini kwa zaidi ya miongo minne amekuwa mmoja wa viongozi wenye ushawishi mkubwa katika siasa za Kenya.
Amegombea urais bila mafanikio, lakini jina lake limekuwa kwenye ulingo wa siasa kwa muda wote.