Mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt Samia Suluhu Hassan amesema mpango wa Serikali yake ni kuhakikisha huduma ya maji safi na salama inakuwa karibu na wananchi na kwamba hatanii katika hilo.
Dkt Samia ametoa ahadi hiyo leo, Jumapili Oktoba 19, 2025 alipozungumza katika mkutano wake wa kampeni za urais, uliofanyika wilayani Sumbawanga katika Mkoa wa Rukwa.
Katika gridi hiyo ya taifa ya maji, amesema analenga vyanzo vikuu vya maji viwe Ziwa Nyasa, Ziwa Tanganyika na Ziwa Victoria, ili kuwa na hifadhi kubwa ya maji.
“Tunapozungumza maji safi na salama hatutanii, tumejipanga kutumia fedha nyingi kufanya gridi ya Taifa ya maji, ili kila Mtanzania awe karibu na huduma ya maji,” amesema Dkt Samia.
#StarTvUpdate