Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, Wakili Albert Msando amewataka wafanyabiashara  kuondoa hofu kuwa Oktoba 29, 2025...

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam, Wakili Albert Msando amewataka wafanyabiashara kuondoa hofu kuwa Oktoba 29, 2025 hakutakuwa na maandamano.

Kwa mujibu Msando, wilaya yake na Mkoa kwa ujumla wamejipanda kuhakikisha amani inatawala siku hiyo.

“Kuna kikundi cha watu wasioitakia mema Tanzania wanatumia mitandao ya kijamii kutaka kuvuruga amani yetu,wanadai kutakuwa na maandamano, niwahakikishe wanajidanganya mimi ni mwenyeki wa ulinzi na usalama wa wilaya niwaambie tumejipanga, ” amesisisitiza Msando.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka wafanyabiashara hao kujiandaa kufanya biashara kama kawaida kwani ulinzi na usalama utakuwa wa kutosha.

Msando ameyasema hayo leo Oktoba 19, 2025 wakati akiwa mgeni rasmi katika kongamano la Shirikisho la wana Vicoba Jijini Dar es Salaam (VICOBA FETA).

#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *