Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Wakili Albert Msando amewataka wazazi kuwakanya watoto wao wasijaribu kushiriki ka...

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Jijini Dar es Salaam Wakili Albert Msando amewataka wazazi kuwakanya watoto wao wasijaribu kushiriki katika maandamano siku ya Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29.

“Niwasihi wazazi, ongeeni na watoto wenu, wasithubutu kujaribu kuandamana. Hatutanii hata kidogo,” amesisitiza mkuu huyo wa wilaya ya Ubungo.

Kwa mujibu wa Msando, kila anayejaribu kuhamasisha maandamano kupitia mitandao ya kijamii vyombo vya usalama vinamfuatilia kwa karibu na akithubutu kufanya hivyo itakuwa fundisho kwa wengine.

“Tuache kujenga hofu kwa wananchi, tarehe 29 watu wakapige kura, hakuna wa kuwasumbua jiji litakuwa shwari, “amesisitiza Msando ambeye alikuwa akizungumza katika kongamano la Shirikisho la Wana VICOBA Jijini Dar es Salaam (VICOBA FETA).

Msando ameongeza kuwa wanaoshawishi Watanzania kuandamana ni kikundi cha watu wachache wanaotumiwa na mabeberu ili kuvunja amani ya nchi na Serikali haiwezi kufumbia macho jambo hiilo.
#StarTvUpdate

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *