Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran amesema: Katika vita vilivyoanzishwa na Marekani na Israel mwezi Juni mwaka huu dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu, adui alipanga kuzusha uvunjifu mkubwa wa amani nchini Iran na alijaribu kutumia magaidi wake wote wakufurushiaji walioachiwa huru huko Syria na Afghanistan kwa ajili ya kuvuruga usalama wa Iran ya Kiislamu lakini alishindwa. Mashirika 50 ya kijasusi yaliisaidia Israel lakini pia yalishindwa.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars, Hujjatul Islam Walmuslimin Sayyid Ismail Khatib amesema hayo kwenye ziara yake ya 85 ya mkoa huko Chaharmahal na Bakhtiari kusini magharibi mwa Iran na kuutaja umoja na mshikamano wa wawananchi na viongozi humu nchini katika Vita vya Siku 12 kwamba ndiyo iliyokuwa sababu kuu ya kupata ushindi Jamhuri ya Kiislamu kwenye vita hivyo. 

Amesema: Maadui walifanya mazoezi mengi kwa ajili ya kuendesha vita hivyo na ndio maana kwenye miaka ya huko nyuma walifanya majaribio mengi ya kuanzisha vita lakini walishindwa. Wamekuwa wakifanya njama zisizosita ikiwa ni pamoja na kujaribu kuwaunganisha wapinzani, wapinga Mapinduzi ya Kiislamu maadui wa Mapinduzi ya Kiislamu kwa kutumia uwezo wote wa vyombo vya habari vya dunia na fedha nyinyi kueneza chuki dhidi ya Iran, chuki dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu na chuki dhidi ya madhehebu ya Kishia lakini daima wanafeli.

Waziri wa Usalama wa Taifa wa Iran pia amesema, adui aliivamia nchi yetu baada ya kujipanga vizuri sana kuongeza kwa kusema: “Kwa taufiki ya Mwenyezi Mungu na kwa busara za Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu na kwa dhamira, umoja na mshikamano wa ndani ya nchi, Iran imepata ushindi kwenye vita hivyo vya siku 12.

Amesema: Adui ambaye anajigamba kuwa na vifaa vyote vya kisasa, ameshindwa kufikia malengo yake hata kwenye eneo dogo tu kama la Ghaza na njama zake pia zinaendelea kufeli huko Lebanon na Syria. 

Waziri Khatib pia amesema, licha ya njama zote za kijasusi zilizofanywa na NATO na mashirika zaidi ya 50 ya kijasusi ambayo yalijipanga kuishambulia Iran kwa njia ya kimya kimya na laini, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tumeshhuhudia ushindi wa taifa la Iran dhidi ya Marekani na utawala wa Kizayuni na waitifaki wao wote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *