Kitendo cha utawala wa kizayuni wa Israel cha kutofungamana na usitishaji vita wa Gaza na kuendelea kuwaua watu wa ukanda huo mdogo kumeuacha mustakabali wa amani katika eneo hilo katika hali tete na isiyoeleweka.
Utawala wa Israel ukiongozwa na Benjamin Netanyahu unauchukulia mpango wa Trump kuhusu Gaza kuwa ni hatua madhubuti ya kuhakikisha usalama wake wa muda mrefu; ambapo kupokonywa silaha kikamilifu kwa muqawama na kutorejea kwa vitisho vya kijeshi ni sharti la kuondoka taratibu kwa vikosi vya Israel kutoka Gaza.
Katika mkutano na waandishi wa habari katika Ikulu ya White House mnamo Septemba 29, 2025, Netanyahu alisisitiza kwamba, Gaza inapaswa kuwa “eneo lisilo na silaha” na eneo la usalama la kudumu. Kinyume chake, Hamas haiuoni mpango huu kama mwisho wa ukaliaji mabavu mabavu, bali kama muendelezo wa satwa ya utawala wa Israel.
Viongozi wa Hamas huko Doha na Istanbul sambamba na kuashiria kutokuweko dhamana ya kuondoka kikamilifu jeshhi la Israel na nafasi finyu ya Mamlaka ya ya Ndani ya Palestina wanaona hiyo ni fura ya mazungumzo. Tofauti hizi, chimbuko lake ni tajiriba na uzoefu wa kihistoria kama vile kushindwa kwa usitishaji mapigano wa 2023 na 2025, ambako kumegeuza usitishaji mapigano kuwa makubaliano yenyye kelegalega.
Ishara hizi zinazokinzana sio tu kwamba zinakwamisha maendeleo ya awamu ya pili ya mpango huo, bali pia zinaandaa mazingira ya mivutano mipya, ambapo utawala wa Kizayuni unatumia vyombo vya habari na diplomasia kuhalalisha misimamo yake. Hatimaye, usitishaji huu wa mapigano unaonekana kuwa wa muda na hatari zaidi.
Visingizio; Sera ya daima ya utawala wa Kizayuni ya kuvunja amani
Moja ya nukta muhimu katika utekelezaji wa usitishaji vita Gaza ni visingizio vya mara kwa mara vya utawala wa Israel kuhusiana na kukabidhiwa miili ya mateka wa Kizayuni.

Kwa mujibu wa makubaliano ya awamu ya kwanza ya mpango wa Trump, Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS inapaswa kurejesha miili ya wafungwa 28 waliokufa ifikapo Oktoba 13, 2025, lakini tisa ilikabidhiwa na mingine iliyobakia ilifunikwa magofu ya Gaza iliyoharibiwa.
Hamas imetangaza kwamba, inahitaji zana maalumu kwa ajili ya kuchunguza vifusi vilivyosababishwa na mashambulizi ya Israel, lakini utawala wa Israel umelitafsiri hilo kuwa ni “kutotekeleza ahadi” na hivyo unakwepa kufungua kivuko cha Rafah kwa ajili ya misaada ya kibinadamu.
Mbinu hii, inayohalalishwa na Netanyahu kama “hatua ya kujihami,” sio tu inakiuka makubaliano lakini pia inazidisha mateso ya raia huko Gaza, ambapo Umoja wa Mataifa umeonya juu ya njaa inayoenea. Hamas pia inaishutumu Israel kwa kutuma miili ya Wapalestina wasiohusiana au kufungwa pingu, mzunguko ambao unatatiza hali hiyo.
Visingizio vya utawala wa Israel vimejikita katika stratijia yake ya kudumisha misimamo ya mazungumzo na kudhihirisha ukosefu wa dhati wa kujenga hali ya kuaminiana. Wakati familia za wafungwa wa Israel zikiandamana mjini Tel Aviv, wakaazi wa Gaza wanakabiliwa na mzozo wa kibinadamu.

Migongano hii inageuza usitishaji mapigano kuwa mchezo wa kisiasa na kupunguza matumaini ya amani ya kudumu, kwani ucheleweshaji wowote husababisha uwezekano wa ukiukaji wa makubaliano.
Kupokonywa silaha muqawama; ndoto za alinacha za utawala wa Kizayuni
Changamoto ya kuipokonya silaha Hamas, kiini cha awamu ya pili ya mpango wa Trump, ni moja ya vikwazo kuu vya hakikisho la usitishaji vita wa Gaza katika muda wa kati. Netanyahu na Trump wanasisitiza juu ya uharibifu kamili wa miundombinu ya kijeshi ya Hamas, ikiwa ni pamoja na njia za chini kwa chini na silaha, wakati Hamas inaliona hilo kuwa ni “kuharibifu wa itikadi na aidiolojia ya muqawama.”
Wataalamu kama vile Hugh Lovatt Baraza la Mahusiano ya Kigeni ya Umoja wa Ulaya wanaonya kwamba Hamas, ikiwa na maelfu ya wanachama wapya waliosajiliwa wakati wa vita, itakataa kupokonywa silaha bila hakikisho la kuuundwa dola la Palestina.
Kwa upande mwingine, mapigano ya hivi karibuni kati ya Hamas na utawala wa Israel huko Gaza yanaashiria jaribio la kurejesha udhibiti, jambo ambalo linakinzana na moyo wa upokonyaji silaha. Changamoto hii sio ya kiufundi tu, bali pia ya kisiasa. Hali hii inageuza usitishaji vita kuwa kipindi cha muda, ambapo Hamas inasalia kuwa tishio la daima kwa utawala wa Israel, kama ilivyokuwa huko nyuma.