#HABARI: Katibu Mkuu wa Wizara ya Utalii na Mambo ya Kale Dkt. Aboud Jumbe amepongeza waandaaji wa Mdahalo wa Hatua 5 za Dkt. Mwinyi, ulioandaliwa na Waandishi wa Habari kutoka Bara na Visiwani, kwa kuonesha mafanikio makubwa yaliyofanyika Zanzibar katika kipindi cha miaka 5 kupitia sekta, wizara na taasisi mbalimbali ambazo zinaongozwa na Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Mratibu Mkuu wa Mdahalo huo, Ndg. Laurent Mwanga (MPISHI CONTENT), amesema kampeni hii imelenga kutathmini na kuelimisha umma juu ya Hatua 5 za Dkt. Mwinyi kama dira ya maendeleo endelevu ya Zanzibar.

Aidha, Ndg. Abdul Halim kutoka Shirika la Bima Zanzibar (ZIC) ametoa pongezi kwa waandaaji na washiriki wote, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika kuibua mijadala chanya ya maendeleo ya taifa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *