Mgombea Ubunge wa Jimbo la Segerea kupitia Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Agnesta Kaiza, ameahidi kuleta mabadiliko chanya na kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa jimbo hilo endapo atapewa ridhaa ya kuwa Mbunge.

Akizungumza katika moja ya mikutano yake ya kampeni, Kaiza amesema atahakikisha anawafuta wananchi machungu waliyoyapata na kuwataka kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kutumia haki yao ya kidemokrasia kumchagua kiongozi wanayemwamini ataweka mbele maslahi ya wananchi.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *