Rais wa Brazil, Luiz InĂ¡cio Lula da Silva, ameukosoa Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa kwa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari ya Israeli dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza, akiamini kwamba vyombo hivi havifanyi kazi yao ipasavyo.

“Nani anaweza kukubali mauaji ya kimbari ambayo yamekuwa yakiendelea kwa muda mrefu katika Ukanda wa Gaza?” da Silva aliwaambia waandishi wa habari huko Putra Jaya jana Jumamosi baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Malaysia, Anwar Ibrahim kabla ya mkutano wa kilele wa ASEAN, ambapo anatarajiwa kukutana na mwenzake wa Marekani, Donald Trump.

Aliongeza kuwa, “Taasisi zilizoanzishwa ili kuzuia mambo kama hayo hazifanyi kazi tena. Leo, Baraza la Usalama na Umoja wa Mataifa hazifanyi kazi tena.”

Kwa kipindi cha miaka miwili, Israel imekuwa katika vita vya mauaji ya kimbari dhidi ya raia wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, na imeua zaidi ya watu 68,000, kurehuri wengine 170,000, na kuharibu karibu 90% ya vifaa na miundombinu.

Matamshi ya Da Silva yanakuja huku uhusiano kati ya Washington na Brasilia ukiboreka kiasi baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu kesi ya rais wa zamani wa mrengo wa kulia, Jair Bolsonaro, mshirika wa Trump ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka 27 jela mwezi Septemba kwa kuhusika kwake katika jaribio la mapinduzi lililoshindwa 2022.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *