Takriban Wamarekani milioni 42 wanakabiliwa na tishio la njaa ikiwa kufungwa kwa shughuli za Serikali ya Shirikisho kutaendelea, na iwapo ufadhili wa SNAP utasimamishwa Novemba 1.

Hiaya yamekuja katika ripoti iliyochapishwa na gazeti la Uingereza, The Guardian.

Ripoti hiyo ilimnukuu Joel Berg, Mkurugenzi Mtendaji wa Hunger-Free America, akisema kwamba ikiwa ufadhili utasitishwa ifikapo mwisho wa mwezi huu, “tutashuhudia janga kubwa zaidi la njaa nchini Marekani tangu Mdororo Mkuu wa Kiuchumi (1930), na sisemi hivyo kama kutia chumvi.”

Gazeti la The Guardian limeeleza kwamba mpango wa SNAP unasaidia familia zinazofanya kazi zenye mishahara midogo, wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 60, na watu wenye ulemavu wanaoishi kwa kipato kisichobadilika.

Tangu kuanza kwa muhula wa pili wa Rais Donald Trump Januari mwaka huu, utawala wake umeanza kampeni ya kubana matumizi ambayo imejumuisha kupunguza maelfu ya ajira za Shirikisho, hasa katika mashirika kama vile Wizara ya Kilimo, Wizara ya Sheria, na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani.

Hatua hizo zimeathiri wafanyakazi wa umma na binafsi, na kusababisha watu wengi kupoteza kipato ghafla bila onyo la awali au fidia ya kutosha. Suala hili limeathiri haraka maisha yao ya kila siku, na sasa baadhi yao wanalazimika kusimama katika safu za benki za msaada wa chakula.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *