#HABARI: Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele, ametembelea na kujionea maandalizi ya ujenzi wa vituo 83 kati ya 90 vya wapiga kura vilivyotengwa maalum kwa wakazi wa zilizokuwa Kata za Ilangu, Ipwaga, Bulamata na Mishamo, zilizopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi, ambapo Kata hizo zilifutwa na Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura ya 287.
Jaji Mwambegele amefanya ziara hiyo katika Kitongoji cha Luhafwe, Kata ya Tongwe, akiwa ameambatana na Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Katavi, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanganyika, na watendaji wengine wa Tume, kwa lengo la kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika Oktoba 29, 2025 nchini kote.
Akizungumza katika eneo la Mnada wa Kitongoji cha Luhafwe, Jaji Mwambegele amesema Tume iliamua kuhamisha baadhi ya vituo vya kupigia kura nje ya makazi ya wakimbizi, na kwamba amefika kuona utekelezaji wa uamuzi huo.
Ameongeza kuwa Tume imetoa matangazo katika maeneo yaliyofutwa na imeweka vituo vipya katika maeneo jirani ili kuhakikisha wananchi wote wanapata haki yao ya kupiga kura.
Kwa upande wake, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Tanganyika, Bi. Kagemlo Mutagwaba, Amesema wapiga kura kutoka Kata zilizofutwa wamehamasishwa vya kutosha na wameonesha utayari mkubwa wa kujitokeza kupiga kura katika vituo vipya vilivyotengwa.
Watanzania wanatarajiwa kupiga kura Oktoba 29, 2025, katika Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani, ukiwa na kaulimbiu “Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura.”
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania