#HABARI: Rais wa Marekani Donald Trump anataka kuigeuza Venezuela kuwa “koloni” la Marekani, Mwanasheria Mkuu wa Venezuela amesema.
Tarek William Saab alisema siku ya Jumapili kwamba wito wa mabadiliko ya utawala nchini Venezuela ni mbinu ya kutaka kunyakua maliasili za nchi yake, ikiwa ni pamoja na akiba ya dhahabu, mafuta na shaba.
Mshirika huyo wa karibu wa Rais wa Venezuela Nicolás Maduro, Saab anasema “hakuna shaka” Marekani inajaribu kuipindua Serikali ya Venezuela, akiongeza kuwa ni jaribio la hivi punde katika msururu mrefu wa majaribio kama hayo “yaliyofeli”.
Marekani ni miongoni mwa mataifa ambayo hayamtambui Maduro kama kiongozi halali wa Venezuela, baada ya uchaguzi uliopita wa 2024 kukosolewa na wengi kuwa haukuwa huru na wa haki.
Trump pia amerudia mara kwa mara uwezekano wa kile alichokiita “operesheni za ardhini” nchini Venezuela, na alisema wiki iliyopita kwamba Marekani “inaangalia uwezekano wa operesheni za ardhini” baada ya kupata udhibiti wa eneo la bahari.”
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania