#HABARI: Soko la Bidhaa Tanzania (TMX) limeendelea kutoa elimu kwa wadau wa sekta ya Korosho nchini, ambapo zaidi ya wanunuzi na wadau 21 wamepatiwa mafunzo kuhusu matumizi ya mfumo wa mauzo ya minada kwa njia ya Kidijitali, mafunzo hayo ni sehemu ya maandalizi ya msimu wa ununuzi wa Korosho kwa mwaka 2025/2026.

Akizungumza katika kikao cha maandalizi ya msimu wa Korosho kilichofanyika leo mkoani Lindi, Afisa Mwandamizi wa Uendeshaji wa Biashara wa TMX, Bi Justa Martine, amesema TMX imefanikiwa kuwafikia wanunuzi na wadau mbalimbali wa sekta hiyo ili kuongeza uelewa kuhusu namna mfumo wa kidijitali wa mauzo unavyofanya kazi.

Bi Martine amebainisha kuwa matumizi ya mfumo huo yamelenga kuongeza uwazi, ufanisi na ushindani katika soko la Korosho, sambamba na kuhakikisha wakulima wananufaika zaidi kupitia bei halisi ya soko.

Ametoa wito kwa waendesha maghala kuhakikisha Korosho zinapangwa na kuhifadhiwa kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyoanishwa na Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), huu akisisitiza kuwa katika msimu huu Korosho zitauzwa kwa kuzingatia ubora uliotambuliwa rasmi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *