#HABARI: Wizara ya Nishati imeanza kutoa elimu kuhusu nishati safi ya kupikia kwa Maafisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia ngazi ya mikoa na halmashauri kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na kuwawezesha Maafisa Dawati kutambua majukumu yao katika utekelezaji wa mkakati.
Akifungua mafunzo hayo, wilayani Kibaha mkoani Pwani, Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani, Bi. Hadija Mruma ameipongeza Wizara ya Nishati kwa jitihada mbalimbali inazochukua kwa vitendo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini mojawapo ikiwa ni kuhakikisha elimu na vifaa vya nishati safi ya kupikia vinafika hadi ngazi za mikoa, halmashauri na vijiji.
Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachi wanatumia nishati safi ya kupikia katika ngazi ya taasisi, kaya n.k akitoa mfano kuwa asilimia 76 ya taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 mkoani humo zimeshahamia kwenye nishati safi ya kupikia.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
 
  
