Azam FC wametinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la CAF baada ya ushindi wa jumla wa mabao 9-0 dhidi ya KMKM kutoka Zanzibar.

Walianza kwa ushindi wa 2-0 ugenini na kumaliza na 7-0 nyumbani Chamazi. Sasa kuelekea mchezo wa mkondo wa pili, Azam FC walitoa fursa kwa mashabiki wao kutunga nyimbo za kusherehek-ea kufuzu hatua ya makundi.

Ni kwamba waliamini fika kwamba KMKM wasingeweza kupindua matokeo ya 2-0 waliyopata ugenini, Oktoba 18. Mashabiki wao kadhaa wakaitikia wito huo na kutunga nyimbo zao na kuzipeleka klabuni.

Baada ya kuzipokea na kuzifanyia tathmini, ukafanyika mchakato wa ndani kuuchagua wimbo bora, na hapo ndipo ‘zali’ likaangukia Mafinga, Iringa.

Vijana watatu kutoka mji huo maarufu kwa baridi na upasuaji mbao, walichaguliwa washindi kwa wimbo unaoitwa AZAM WALE PALE.

Vijana hao ni John Cico maarufu kama DJ Cico, Cyprian Kabogo maarufu kama Sipro TZ, na Daniel Christian maarufu kama Mr Magic ambaye pia ndio mtayarishaji yaani producer.

Wakatunga wimbo kisha wakafunga safari kutoka Mafinga hadi Chamazi kupeleka wimbo wao.

Ukapokelewa na baada ya mchakato ndipo ukachaguliwa kuwa wimbo bora na hapo ndipo kwenye picha kamili!

Azam FC ikataka kuununua wimbo huo ili kuumiliki kihalali kuepuka mambo ya haki miliki na mirabaha, ikawauliza tha-mani yake.

Wao wakajibu kwamba hawakutunga wimbo huu kwa ajili ya biashara bali mapenzi yao kwa Azam FC, kwa hiyo ha-wauuzi bali wanautoa kama zawadi kwa klabu yao pendwa.

Mabosi wa Azam wakapenda sana majibu yao na katika mazungumzo zaidi wakatokea katika eneo ambalo linaweza kubadilisha maisha ya vijana wale.

Ni kwamba hawa vijana wana ndoto ya kujiajiri kwenye muziki, wana studio yao huko Mafinga, na ndio waliyorekodia wimbo huo.

Lakini vifaa vyao vimechakaa na hawana uwezo wa kupata vifaa vingine. Mabosi wakauliza bei ya vifaa hivyo wakatajiwa na kuahidi kuwasaidia.

Kwa hiyo vijana hawa watapata vifaa vipya kwa hisani ya mabosi wa klabu yao pendwa. Mabosi watatoa vifaa kwa upendo kama vijana walivyoutoa wimbo kwa upendo.

Hata hivyo, ili kuepuka mikanganyiko ya kisheria huko mbele, klabu iliwaomba vijana hao kuingia nayo mkataba wa makabidhiano ya wimbo huo.

Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Azam FC, Zaka Zakazi, aliyekuwa akiambatana na vijana hao katika ziara za kwenye vyombo vya habari, amethibitisha kwamba ni kweli klabu na wasanii hao wamesaini mkataba wa maka-bidhiano ya wimbo huo.

“Ni kweli, ni lazima wimbo huu utambulike kisheria kwamba ni mali ya Azam FC kwa sababu hii ni taasisi na haipaswi kufanya mambo bila maandishi.”

Muimbaji kinara, Cyprian Kabogo maarufu kama Sipro TZ, anasema kimsingi wimbo huu waliutunga siku nyingi sana, ila safari hii ni kama wameuhuisha tu (Remix).

“Mara ya kwanza tulitunga wimbo kuzungumzia biadhaa zote za kampuni mama ya Azam.”

Sipro anasema wimbo huo unapatikana hata kwenye Instagram kwa sababu waliuweka huko kama sehemu ya kuutangaza.

“Kwa hiyo tuliposikia kuna fursa ya wimbo mpya, tukaona tuurudie uleule ila tuizungumzie klabu pekee, na kweli, umepokelewa vizuri”.

Sipro anasema wimbo huu umewatangaza sana kwani wamepata nafasi ya kufanya mahojiano kwenye vipindi vya redio mbalimbali kubwa za Dar es Salaam.

“Wimbo wetu umekubalika sana, hata pale uwanjani siku ya mchezo wetu na KMKM, watu tuliokaa nao karibu walikuwa wanausifia bila kujua kama sisi ndio waimbaji,” alisema DJ Cico.

Mtayarishaji wa wimbo huo, Daniel Christian maarufu kama Mr Magic, anasema zaidi ya yote wimbo huo umewasaidia kupata mawasiliano na wadau wengi wa muziki mjini Dar es Salaam.

“Unajua Dar es Salaam ndio mbuga kuu ya kila mmoja kuja kuwinda mnyama amtakaye, kwa hiyo sisi pia tumepata nafasi ya kuwawinda na kuwapata wanyama tunaowataka kutokana na wimbo huu.”

Baada ya kutambulishwa na mafanikio ya wimbo huu, sasa wanataka kulivamia soko rasmi kwa kuja na nyimbo kali mfululizo.

“Kwa kweli ukosefu wa vifaa vya studio ulitukwamisha sana, lakini milango inaanza kufunguka. Vyombo tunapata na jina letu linakuana tunapata mawasiliano na watu muhimu sana.”

Ukurasa huu ukataka kujua kutoka kwa Azam FC juu ya mipango ya kuufanya wimbo huu udumu, kwa sababu unaon-ekana umetungwa maalumu kwa hatua ya makundi tu.

Na pia umetaja majina ya wachezaji kiasi kwamba wakiondoka na wimbo unakosa mashiko.

Zaka Zakazi akasema wimbo huu ni maalumu kwa ajili ya kufuzu makundi lakini wameshafanya mazungumzo na wa-tunzi waandae wimbo mwingine kwa kutumia wimbo huu huu, bila kutaja majina au matukio yanayoisha.”.

“Wao wenyewe wamesema watatunga wimbo, au tuseme wataufanyia marekebisho wimbo huu ili uweze kutumika nyakati zote”, alisema Zaka Zakazi.

Hata hivyo Zaka amesema hadi sasa klabu haina wimbo wake rasmi kama zilivyo klabu kadhaa duniani.

“Tupo kwenye mchakato wa kupata wimbo rasmi utakaotambulisha klabu kama Real Madrid na Hala Madrid, au Chel-sea na Blue is the Colour”.

Azam FC ni klabu iliyoanzishwa mwaka 2004 na kupanda ligi kuu mwaka 2008.

Ilianza kushiriki mashindano ya Afrika mwaka 2013 na kupitia nyakati nyingi za kuumizwa kwenye mashindano haya.

2013 – Kombe la Shirikisho

Walitolewa raundi ya pili na FAR Rabat ya Morocco kwa kipigo cha ugenini cha 2-1 baaada ya suluhu Benjamin Mkapa. 2014 – Kombe la Shirikisho  Walitolewa raundi ya awali na Ferroviário da Beira ya Msumbiji kwa matokeo ya jumla ya 2-1.

Walishinda 1-0 Chamazi na kufungwa 2-0 ugenini. Huu ndio ulikuwa msimu wa kwanza kuutumia uwanja wao kwenye mashindano ya CAF. 2015 – Ligi ya Mabingwa  Walitolewa raundi ya awali na El Merreikh ya Sudan kwa matokeo ya jumla ya 3-2.

Walishinda 2-0 nyumbani na kufungwa 3-0 ugenini. 2016 – Kombe la Shirikisho  Walitolewa na Esperance (Taraj) ya Tunisia kwa matokeo ya jumla ya 4-2.

Walishinda 2-1 nyumbani na kupoteza 3-0 ugenini. 2017 – Kombe la Shirikisho  Walitolewa raundi ya kwanza na Mbabane Swallows F.C. ya Eswatini kwa matokeo ya jumla ya 3-1.

Walishinda 1-0 nyumbani na kufungwa 3-0 ugenini. 2018 – hawakushiriki 2019 – Kombe la Shirikisho  Walitolewa raundi ya kwanza na Triangle ya Zimbabwe kwa matokeo ya jumla ya 2-0.

Walifungwa 1-0 nyumbani na ugenini. 2020 – hawakushiriki 2021 – Kombe la Shirikisho

Walitolewa raundi ya kwanza na Pyramids ya Misri kwa kipigo cha 1-0 cha ugenini baada ya suluhu nyumbani. 2022 – Kombe la Shirikisho

Walitolewa raundi ya awali na Al Akhdar ya Libya kwa matokeo ya jumla ya 3-2. Walipoteza 3-0 ugenini na kushinda 2-9 nyumbani. 2023 – Kombe la Shirikisho

Walitolewa raundi ya kwanza na Bahir Dar Kenema ya Ethiopia kwa mikwaju 4-3 ya penalti baada ya sare ya 3-3 kwenye matokeo ya jumla.

Walipoteza 2-1 ugenini na kushinda 2-1 nyumbani. 2024 – Ligi ya Mabingwa Walitolewa raundi ya awali na APR ya Rwanda kwa matokeo ya jumla ya 2-1. Walishinda 1-0 nyumbani na kupoteza 2-0 ugenini Wacha washangilie, kama unavyosikika wimbo wao bora waliouchagua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *