Mgombea ubunge wa Jimbo la Arusha Mjini kupitia CCM, Paul Makonda, ameahidi kujenga barabara ya juu (flyover) na barabara za njia nne katika maeneo yenye msongamano mkubwa jijini Arusha, endapo atachaguliwa kuwa mbunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Akihitimisha kampeni zake leo, Jumatatu, katika Stendi Kuu ya Arusha, Makonda amesema kuboresha miundombinu ni kipaumbele chake kikuu ili kupunguza foleni na kuinua hadhi ya jiji hilo.
Amesisitiza kuwa mpango huo uko kwenye ilani ya CCM, na ameahidi kusimamia utekelezaji wake mara baada ya kupewa ridhaa ya wananchi.
✍ Mwandishi Wetu
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates