Serikali imeendelea kuibua matumaini mapya kwa wakulima waliokuwa wakijihusisha na kilimo cha mazao haramu kama bangi na mirungi, kwa kuwawezesha kuingia kwenye kilimo cha mazao halali yenye tija.
Kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), serikali inatekeleza programu ya mazao mbadala inayolenga kuwainua wakulima kiuchumi, kuimarisha usalama wa chakula, na kulinda utu wao kama raia wenye mchango katika maendeleo ya taifa.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Fatma Nyangasa amesema hatua hii imekuwa ishara ya mabadiliko chanya yanayoleta suluhu ya kudumu badala ya adhabu, huku ikiibua kizazi kipya cha wakulima wanaochangia uchumi wa halali na endelevu.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi
