Serikali mkoani Mara imeliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoani humo kufanya ukaguzi katika majengo ya serikali na majengo yanayoendelea kujengwa ili kubaini usalama wa mifumo ya kupambana na majanga ili kudhibiti athari za majanga yanayohusu moto.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi ameyasema hayo mapema leo wakati akikabidhi magari manne kwa jeshi hilo.
Imeandaliwa na Augustine Mgendi
Mhariri @moseskwindi