Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limeonya kwamba uharibifu unaoendelea ambao umeaosababishwa na vita vya Israel katika eneo la Ukanda wa Gaza huko Palestina, ikiwa ni pamoja na uharibifu wa miundombinu ya elimu, umeweka mustakabali wa mamilioni ya watoto wa Kipalestina hatarini.

Baada ya safari ya kutembelea Ukanda wa Gaza, Mkurugenzi wa Kanda ya Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini wa UNICEF, Edouard Beigbeder, ametangaza kuwa: “Huu ni mwaka wa tatu mfululizo ambapo watoto wa Gaza wameachwa bila shule, na bila hatua za haraka, kizazi kizima kitapotea.”

Beigbeder ameongeza kuwa: “Asilimia 85 ya shule za Gaza zimeharibiwa au hazitumiki tena, na shule nyingi zilizobaki zimegeuzwa kuwa makazi ya watu waliokimbia makazi yao; na kujenga upya shule hakuwezekani bila vifaa vya ujenzi.” Amesema vifaa vya msingi kama vile madawati na vitabu havipatikani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Wizara ya Elimu ya Palestina, zaidi ya wanafunzi 20,000 wameuawa shahidi na makumi ya maelfu kujeruhiwa tangu kuanza mauaji ya kimbari ya Israel Oktoba 7, 2023; takwimu inayofichua ukubwa wa janga la binadamu katika Ukanda wa Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *